Hatua za kufanya Setup ya Email kwenye simu ya Android. Pia, unaweza kuangalia video kwa kwenda Hapa
1. Bonyeza Setting kwenye simu yako
2. Baada ya kubonyeza Settings, nenda kwenye Applications na uchague Email
3. Kama ulikuwa haujawahi kutengeneza email kwenye simu, utaulizwa utengeneze mpya, na kama ulikuwa umeshaitengeneza, basi chagua kutoka kwenye orodha ya emails
4. Ingiza username (email kamili, mfano info@websitename.com) na uingize Password ya email. Kumbuka password hii inapatikana kwenye CPanel, kama bado haujatengeneza email, tafadhali pitia video hii. Ili kuhakikisha unaingiza Password isiyokosewa, unaweza chagua show password.Unatakiwa uchague Manul Setup inayoonekanika chini, siyo Next
5. Ukishabonyeza manual Setup, kutatokea machaguazi matatu, chagua IMAP Account
6. Kutatokea kidirisha cha Incoming Server Settings, unatakiwa kuhakikisha umeingiza taarifa zote kama inavyoonekana kwenye picha (Username na Email Address ni email address yako mfano info@jinalawebsite.co.tz). MUHIMU: Hakikisha umebadili IMAP Server kutoka iliyopo na kuwa 198. 57. 207. 196 bila nafasi kati ya namba, na kwenye Security Type chagua None. Kisha bonyeza Next
7. Ukishabonyeza Next, kutafunguka kidirisha cha outgoing Server Settings, hapa utahakikisha unafuata Picha ya pili kulingana na taarifa zako. SMTP Server tumia 198. 57. 207. 196 na kwenye Security Type chagua SSL (Accept all Certificates) bila kusahau umechagua Require Sign-in. Port number tumia 587 kama simu haijaandika (mara nyingi hujiandika)
Picha ya kwanza muonekano kabla ya Setting, picha ya pili ni muonekno baada ya kuweka settings zinazotakiwa kwa email yako ifanye kazi. Baada ya hapo bonyeza Next
8. Kama umeingiza taarifa zote kwa uhakiki, hadi hapo utaweza kuconnect na Servers za Dudumizi, na utapata ujumbe huu chini, changua kulingana na unavyopenda halafu bonyeza Next.
9. Hadi hapa umeshamaliza, kwa mara ya kwanza emails hazitoweza kuonekana, unatakiwa kubonyeza load more emails
Hizo ndizo hatua muhimu kuweza kusetup email kwenye simu yako ya mkononi. Pia, unaweza kuangalia video kwa kwenda Hapa